Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Marekani ameonya kuwa mgogoro unaohusishwa na Iran unaweza kugeuka kuwa “Vietnam ya Trump,” akitoa tahadhari kuhusu hatari za kuendelea kwa mivutano ya kijeshi.
Ameeleza kuwa kama ilivyotokea Vietnam, ambapo Marekani ilihusika katika mazungumzo lakini hatimaye ilikabiliwa na mabadiliko makubwa ya uwanja wa vita, hali kama hiyo inaweza kujirudia katika muktadha wa sasa.
Aidha, ameonya kuwa endapo hakutafikiwa makubaliano thabiti, kuna uwezekano wa mkataba dhaifu na usio imara, hali ambayo inaweza kusababisha Marekani na washirika wake, akiwemo Israel, kujikuta wakihitajika tena kuhusika kijeshi na Iran katika miaka ijayo.
Your Comment